TaCCIRe Repository

Miti ya matunda kwa hifadhi ya mazingira na stahimili ya mabadiliko ya tabia nchi

Show simple item record

dc.contributor.author Kusolwa, P.M.
dc.contributor.author Mgembe, E.R.
dc.contributor.author Mwaitulo, S.
dc.date.accessioned 2013-02-14T08:46:32Z
dc.date.available 2013-02-14T08:46:32Z
dc.date.issued 2012-03
dc.identifier.citation Kusolwa, P.M. et al. (2012). Miti ya matunda kwa hifadhi ya mazingira na stahilmili ya mabadiliko ya tabia nchi en_GB
dc.identifier.uri http://www.taccire.sua.ac.tz/handle/123456789/55
dc.description FRUIT TREES -CLIMATE CHANGE - ADAPTATION en_GB
dc.description.abstract Kilimo ni uti wa mgongo wa mkulima vijijini. Kulingana na kukua kwa familia, kupungua kwa rutuba na mabadiliko ya mahitaji ya wakulima vijijini wakulima wameendelea kufungua mashamba mapya ili kuongeza mavuno na kipato. Upanuzi huu wa mashamba mara nyingi huambatana na kukatwa kwa miti au misitu. Hali hii inaleta ukame na ongezeko la joto katika maeneo husika. Ukataji wa miti kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa mashamba ya mazao hasa ya chakula yanahusishwa na dalili kubwa za mabadiliko ya tabia nchi. Jitihada nyingi zimefanyika ili kuhamasisha wananchi kuhifadhi mazingira kwa kampeni za kupanda miti na kuhamasisha wananchi kutokata miti bila kupanda mti. Hata hivyo mwongozo huu, mara nyingi hulenga miti ya misitu peke yake. Kitabu hiki kinatoa mwongozo wa mbinu za ustawishaji wa miti ya matunda kama njia nyingine ya kuhifadhi mazingira na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi. Kulingana na tafiti zilizofanyika juu ya miti ya misitu, inatarajiwa kwamba miti ya matunda pia itasaidia kupungua hewa ya ukaa, kupunguza ongezeko la joto, na kuboresha mkusanyiko wa mawingu ya mvua, kuimarisha utunzaji wa maji aridhini katika maeneo ya mashambani. Zaidi ya yote, mit ya matunda itasaidia kuongeza uhakika wa chakula na kipato cha kaya vijijini. Kwa kuwa miti ya matunda itakuwa na thamani kubwa kwa familia, hivyo si rahisi kukatwa kwa matumizi mengine (kama vile kuni au mkaa). Hivyo basi elimu ya uzalishaji wa miche na utunzaji mzuri wa bustani za matunda ni muhimu ili kuweka mazingira mazuri ya uoto wa kijani, kuhifadhi ardhi na kujihami na mabadiliko ya tabia nchi. Kitabu hiki kinatoa maelezo ya mbinu bora za uzalishaji wa miche na ustawishaji wa Miparachichi, Miembe, na Michunga. Chimbuko la kazi hii ni moja ya miradi inaloyenga utekelezaji wa shughuli za mpango mpya unaohusu hifadhi ya mazingira na stahimili ya mabadiliko ya tabia nchi (Climate Change Impacts Adaptation and Mitigation - CCIAM). en_GB
dc.language.iso other en_GB
dc.publisher SUA, MOROGORO en_GB
dc.subject ADAPTATION, CLIMATE CHANGE en_GB
dc.subject MANGOE - TREES en_GB
dc.subject MANGOES en_GB
dc.subject AVOCADO -TREES en_GB
dc.subject AVOCADO en_GB
dc.subject ORANGE -TREES en_GB
dc.subject ORANGES en_GB
dc.subject FRUITS TREES en_GB
dc.title Miti ya matunda kwa hifadhi ya mazingira na stahimili ya mabadiliko ya tabia nchi en_GB
dc.type Book en_GB


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search TaCCIRe


Browse

My Account